Vifahamu vyakula vinavyoweza kukuondolea nguvu za kiume

2240
0
Share:
Share this
  • 1.7K
    Shares
CMTL Group

Kulingana na Jarida mashuhuri la Wataalamu wa Tiba nchini Marekani (The American Journal of Medicine) aina ya vyakula unavyokunywa au vinywaji na aina ya maisha vina mchango mkubwa katika afya yako ya uzazi. Kutoka katika jarida hilo, tumekukusanyia baadhi ya vitu ambayo vinaweza kukusababishia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Vinywaji baridi vilivyosindikwa (carbonated)

Unywaji wa vinywaji vya aina hii umeonekana kuwa kwa kiasi kikubwa hupunguza uwezo wa mbegu za kiume kuogelea (motility) kwenda katika kurutubisha yai la kike.

Kunywa pombe kupita kiasi

Unywaji wa pombe kupita kiasi ni sababu nyingine ambayo imetajwa kuwa tishio kwa afya ya uzazi na nguvu za kiume. Kadiri kiwango cha pombe (alcohol) kinavyozidi katika damu ndivyo kiwango au wingi wa mbegu za kiume zenye nguvu unavyopungua (sperm count)

Nyama za makopo au za viwandani

Utafiti wa jarida hilo umeeleza kuwa wanaume wanaotumia nyama za makopo au viwandani kwa kiwango kikubwa wana mbegu za kiume zenye upungufu wa ubora wa hadi asilimia 23 kulinganisha na wale wasiotumia vyakula hivyo.

 

Cheese na Full Fat Milk

Kulingana na utafiti huo, vyakula vinavyotokana na bidhaa za maziwa na maziwa kwa ujumla husaidia kuongeza proteni lakini matumizi yake kuzidi kiwango hasa Full Fat Milk huleta athari hasi kwa ukuaji na wingi wa mbegu za kiume.

 

 

Comments

error: Content is protected !!