Vilabu 4 vya Uingereza vinavyowania kumsajili Mbwana Samatta

363
0
Share:
Share this
  • 544
    Shares

Mshambuliaji wa kimataifa kutoka Tanzania anayekipiga na klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji anahusishwa kujiunga na klabu mbalimbali za nchini Uingereza ikiwemo Everton, West Ham United, Burnley na Brighton & Hove Albion.

Samatta ambaye nyota yake imezidi kung’aa vizuri msimu huu, tayari ameshazifumani nyavu mara 8 katika michezo 11 aliyoichezea klabu yake msimu huu.

Klabu ya Everton bado inakumbwa na tatizo kubwa la mshambualiaji baada ya Romelo Lukaku kujiunga na mashetani wekundu (Manchester United) mwaka 2017 kwa ada ya uhamisho ya shilingi bilioni 224.

Everton tayari imekuwa na muunganiko fulani na vilabu vya soka Afrika Mashariki ambapo kwanza, inadhaminwa na Sportpesa, lakini ni timu pekee ya ligi kuu ya Uingereza ambayo imecheza mechi Afrika Mashariki. Timu hiyo ilikipiga na Gor Mahia ya Kenya katika dimba la taifa Dar es Salaam.

Lakini itakuwa klabu ya kwanza ya Uingereza kuialika klabu kutoka Afrika Mashariki.

 

Comments

error: Content is protected !!