Wasifu wa Waziri mpya wa Mambo ya Ndani Kangi Alphaxard Lugola

1536
0
Share:
Share this
  • 1K
    Shares
CMTL Group

Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo Julai 1 2018, amefanya mabadiliko madogo katika Baraza lake la Mawaziri. Pamoja na mabadiliko mengine, Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt Mwigulu Nchemba ameondoshwa katika nafasi yake na badala yake ameteuliwa Mbunge wa Mwibara Kangi Alphaxard Lugola kuchukua nafasi yake. Kutokana na unyeti wa Wizara hiyo, hapa chini tumekuwekea wasifu mfupi wa Waziri huyo mpya wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kangi Lugola ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara mkoani Mara kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.

Amezaliwa Mei 25 mwaka 1963, ikimaanisha sasa ana umri wa miaka 55. Alipata elimu yake ya msingi katika shule za Nyamitwebili kati ya mwaka 1974 to 1977, kabla ya kuhamia Shule ya Msingi Mugeta mwaka  1978 na baadaye kwenda Shule ya Msingi Kavunjo alikohitimu Shule ya Msingi. Kati ya mwaka 1981 hadi 1984 alikuwa mwanafunzi wa O Level Shule ya Sekondari Sengerema. Baadaye aliendelea na A Level katika Shule ya Sekondari ya Wavulana Songea (Songea Boys) na kuhitimu mwaka 1987.

Kangi Lugola ni mhitimu wa Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1988-1992) na pia mhitimu wa mafunzo baada ya Shahada ya awali (Postgraduate) toka Chuo Kikuu cha Leicester nchini Uingereza.

Alianza siasa mwaka 1986 na amekuwa Mbunge wa Mwibara toka mwaka 2010. Kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira.

 

Comments

error: Content is protected !!