Watumiaji wa iPhone waiburuza mahakamani kampuni ya Apple

654
0
Share:
Share this
  • 364
    Shares

Kampuni ya Apple imewadanganya wateja wake kwa kupunguza uwezo wa kiutendaji (slowdown) wa simu za iPhone pasipo kuwataarifu  wateja wake, hii ni kwa mujibu wa mashtaka nane yaliyofikishwa katika Mahakama, nchini Marekani ikiwa ni wiki moja tu tokea kampuni hiyo ikiri kufanya hivyo.

Mabadiliko hayo yaliyofanywa na kampuni ya Apple yanaweza kuwa yaliwapotosha baadhi ya wateja wakati wakijaribu kutafuta mbinu za kutatua tatizo hilo mwaka uliopita, yalidai mashtaka hayo.

Mashtaka yote yaliyowasilishwa katika Mahakama za Wilaya katika majimbo ya California, New York na Illinois yana lengo la kutaka kuwakilisha watumiaji wa simu zaiPhone walioko katika maeneo mbalimbali.

Gazeri la Haaretz limeandika kuwa kesi kama hiyo hiyo imeripotiwa katika Mahakama nchini Israel.

Wiki iliyopita, Kampuni ya Apple ilikiri kuwa imepunguza uwezo wa kiutendaji wa simu za iPhone kwa matoleo ya iPhone 6, 6S, SE, na 7, kutokana na kupungua kwa ubora wa utendaji wa betri.

Comments

error: Content is protected !!