Watumishi wa umma waonywa kuhusu kunywa chai asubuhi

857
0
Share:
Share this
  • 2.3K
    Shares
CMTL Group

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amewataka watumishi wa umma kuacha mara moja tabia ya kutumia muda mwingi kunywa chai na kusababisha kuchelewa kuwahudumia wananchi wanaofika katika ofisi zao kwa ajili ya kutatuliwa matatizo yao.

Waziri Mkuchika amesema katika ofisi nyingi za serikali, wananchi hukaa muda mrefu wakisubiria huduma hasa muda wa chai na chakula cha mchana kutokana na watumishi kutumia muda mwingi wanapokwenda katika migahawa.

Mkuchika alibainisha hayo alipokuwa akikabidhiwa ofisi na waziri aliyekuwa akishikilia wadhifa huo, Angellah Kairuki ambaye sasa ni Waziri wa Madini.

Mkuchika aliwaonya watumishi wote kuwa, wasiopoacha tabia ya kuchelewesha huduma kwa wananchi, watachukuliwa hatua kali.

Aidha, amezitaka ofisi za umma kufungua migahawa katika maeneo ya ofisi hizo ili kurahisisha huduma ya chakula kwa watumishi, na iwapo hawawezi, basi watangaze zabuni.

Alisema, kushindwa kuwahi kutoa huduma kunasababishwa na mambo mengi mojawapo likiwa ni hilo la kunywa chai, lakini akaeleza kuwa, muda mwingine migahawa yenyewe ipo mbali kwa hivyo watumishi wanatumia muda mwingi kwenda na kurudi ndio sababu ameagiza ofisi za umma ziwe na migahawa ya kutolea huduma.

Comments

error: Content is protected !!