Wawakilishi wa Kamati ya Kutetea Waandishi wa Habari (CPJ) wakamatwa Tanzania

304
0
Share:
Share this
  • 47
    Shares

Kamati ya Kuwalinda Waandishi wa Habari (Committee to Protect Journalists-CPJ) imezitaka Mamlaka nchini Tanzania kuwaachia huru wawakilishi wake wawili barani Afrika,  Angela Quintal, ambaye ni Mratibu wa Progamu Afrika na Muthoki Mumo ambaye nu Mwakilishi wa CPJ Kusini mwa Jangwa la Sahara ambao wanadaiwa kukamatwa na maofisa waliojitambulisha kuwa wanafanya kazi na Idara ya Uhamiaji.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa katika tovuti ya CPJ, maafisa hao walifika katika hoteli ambapo wawakilishi hao walikuwepo na kuwaweka chini ya ulinzi, huku wakipekua mali zao ambapo walichukua hati zao za kusafiria (passport) ambazo bado wanazishikilia.

Quintal na Mumo baada ya hatua hiyo na upekuzi walichukuliwa na maafisa hao kutoka hotelini na kupelekwa sehemu ambayo bado haijafahamika.

Wawakilishi hao walikuwa nchini ambapo walikuwa akitekeleza majukumu ya CPJ.

“Tuna wasiwasi kuhusu usalama wa wenzetu Angela Quintal na Muthoki Mumo, ambao wanashikiliwa angali wapo Tanzania kihalali,” alisema Joel Simon, Mkurugenzi Mtendaji wa CPJ.

Mkurugenzi huyo amezitaka mamlaka za Tanzania kuwaachia haraka wawakilishi hao na kurejesha hati zao za kusafiria.

Aidha, kwa mujibu wa Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa amewasiliana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kuhusu sakata hili, lakini waziri huyo mwenye dhamana ameonesha kutokufahamu chochote kuhusu wawakilishi hao kukamatwa.

Waziri Lugola ameahidi kuwa anafuatilia taarifa hizo.

Comments

error: Content is protected !!