Wema Sepetu afungiwa kwa muda usiojulikana

382
0
Share:
Share this
  • 413
    Shares

Bodi ya Filamu Tanzania imemfungia muigizaji Wema Sepetu kutojihusisha na filamu na uigizaji kwa muda usiojulikana baada ya kusambaa kwa picha na video zake zenye maudhui ya kingono mitandaoni.

Adhabu hiyo imetolewa leo Oktoba 26 wakati mrembo huyo aliyetwaa taji la Miss Tanzania mwaka 2006 alipoitwa na bodi hiyo kwa ajili ya kuhojiwa.

Bodi hiyo imesema kuwa imemfungia msanii huyo hadi pale itakapojiridhisha kuwa amebadilika na kwamba itakuwa ikifuatilia mwenendo wake kwa karibu.

Aidha, bodi hiyo imesema kuwa, mtu yeyote atakayeshiriki kwa namna yoyote ili, au kuonesha au kusababisha kuoneshwa kwa picha au video zinazokinzana na masharti ya filamu, atakuwa amekiuka Kanuni za Sheria ya Filamu ya mwaka 1976

Wakati Wema akiangushiwa adhabu hiyo, msanii Amber Rutty ambaye naye video zake zenye maudhui hayo zikiwa zimesambaa mitandaoni, ametakuwa kuripoti katika kituo chochote cha polisi na akifika hapo atapata ujumbe wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

RC Paul Makonda ametoa agizo hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika “Wakati TCRA wakijipanga kuchukua hatua, mimi namtaka mwenye picha hii kufika kituo chochote Cha Polisi kilichopo karibu na eneo lake kabla ya 12 jioni. Na ukifika waambie umeitwa na Rc Makonda watakupatia ujumbe wako.”

Comments

error: Content is protected !!