Zijue maana za ‘tick’ katika mtandao wa WhatsApp

811
0
Share:
Share this
  • 951
    Shares

Mtandao wa kijamii wa WhatsApp umekuwa ni moja kati ya mitandao maarufu sana inayotumiwa na watu wengi duniani. Siyo vijana tu kama ilivyozoeleka kuwa ndiyo wapenzi wa mitandao ya kijamii, bali hata watu wazima na wazee.

WhatsApp imekuwa ikijitahidi kuborosha mtandao wake kadiri siku zinavyokwenda ili uweze kukidhi mahitaji ya watumiaji wake katika maeneo mbalimbali duniani.

Tangu mtandao huu ulipopata maboresho ambayo yanamwezesha mtumiaji kugundua kama ujumbe wake umefanikiwa kutumwa, umepokelewa na kusomwa na mpokeaji, jambo hili kwa baadhi ya watu limekuwa la kufurahisha huku wengine wakipata maudhi kutokana na kuona jumbe zao zimesomwa na hawajibiwi.

Wengine nao ili kuepuka adha hii, wamefikia uamuzi wa kuficha vema (ticks) zinazoonyesha kuwa ujumbe umesomwa.

Hizi hapa ni maana na vema (tick) katika mtandao wa whatasapp.

Unapotuma ujumbe kupitia ‘whatsApp’ ikitokea alama moja ya vema yenye rangi ya kijivu hiyo huwa na maana kuwa ujumbe wako umefanikiwa kwenda lakini bado haujamfikia mlengwa au mpokeaji.

Wakati mwingine unaweza kutuma ujumbe halafu ukaona alama kama ya duara, alama hiyo huwa inamaanisha kuwa ujumbe wako bado haujafanikiwa kutumwa na inawezekana ikawa ni ubovu wa mawasiliano au hauna kifurushi cha data kitakachokuwezesha kuutuma ujumbe huo.

 

Pale ambapo ujumbe utafika katika simu ya mpokeaji ile alama ya vema itabadilika na kuwa vema mbili za rangi ya kijivu.

Ujumbe unapoingia katika simu ya mpokeaji na kusomwa ama tu kufunguliwa, basi alama ile ya vema mbili hugeuka na kuwa ya rangi ya bluu.

Hapa kama uliyemtumia ujumbe hatokujibu, siyo kwamba hajaupata na kuusoma ujumbe wako, bali yawezekana hataki kukujibu au anafanya vitu vingine ambavyo vinamzuia yeye kukujibu kwa wakati huo.

Comments

error: Content is protected !!